Hatuwezi kuendelea kukaa kimya. Taifa letu linaaibika vibaya sana.

Wahusika wanajulikana. Wametajwa mara nyingi na mbinu wanazozifanya kwa kutumia wasanii wa kizazi kipya na waigizaji almaarufu kama 'Bongo Movie'.

Inaudhi, inakera na inatuongezea chuki sana kwa serikali iliyo madarakani. Kaeni kimya na endeleeni kulichafua taifa, kuna siku mtatueleza yote. Au kwakuwa wahusika ni wanenu? Au kwakuwa wakuu wa juu ni wale waliowawezesha kuingia madarakani kisiasa?

Ndugu zangu, hii ni aibu kubwa kwa Taifa. Inasikitisha sana na inazidi kutuaibisha wengine tunaosafiri ng'ambo. Taifa kama halina rais, taifa kama halina Vyombo vya Dola. Ni upumbavu, ni ufedhuli na mtambue sasa tumechoka. Sasa, tunaanza kuziweka habari za kila anayekamatwa na madawa hadharani, tunaanza kuweka hadi wanaowatuma. Tutawafikia mapapa wote!

Mambo haya mlimchomekea mtoto wa Mengi, mambo haya mnawachomekea wanyonge wenye njaa kali na hadi mmeua vijana wetu kwa kuwabebesha mizigo michafu hivi!

Kwa ambao hamjasoma habari hii ya aibu, someni hapa:

Wanawake wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
Someni zaidi hapa Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa



USHAURI KWA VIJANA WA KITANZANIA:
Quote By Kamundu View Post
Hakuna mtu asiyependa utajiri lakini utajiri unaweza kupatikana bila kufanya biashara haramu au kujihusisha na mambo ya kuhatarisha maisha yako. Kwa miaka ya karibuni kumekuwa na Watanzania wengi wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na wanaofaidika ni wachache tu wengi wao wanaishia kupata pesa ndogo na wanahatarisha maisha yao kwa kufugwa, kifungo cha kifo na hata madawa kupasuka tumboni na kuwaua. Kabla hujapata utajiri wa kudumu unatakiwa kupenda maendeleo kwanza na sio sifa pekee kwenye jamii. Fanya yafuatayo na polepole utafanikiwa.

1. Tafuta mtu ambaye unataka kuwa kama yeye: Usiangalie ukabila udini wala rangi ya mtu. Kama unataka kuwa kama Mengi, Mkono, Manji, Wanasiasa, wasomi au hata wasomi wa kimataifa wanaofanya kazi kwenye UN, World bank, diasporas. Tafuta mtu mmoja au wawili na waombe wawe kama walimu wako. Usiogope kutafuta utapata mtu na fuata wanayo kuambia hata kama wewe huoni umuhimu kwa sasa.

2. Jiendeleze kielimu: Hakuna mtu ambaye hawezi kufanya hili hata kama ni polepole. Elimu sio lazima iwe ya degree kwani duniani sasa kazi zinazolipa hazifundishwi kwenye degree bali certification mfano sasa tuna gas jifunze ufundi wa machine za kuchimba mafuta, project management, computer language, database kama SAP,Oracle, dot.net. Vilevile kuna Veta tafuta kitu ambacho kinauhusiano na Gas na Oil. Kwa ujumla jiwekee utamaduni wa kujiendeleza.

3. Marafiki: Tafuta marafiki ambao wanakusaidia kujiendeleza na wanakupenda badala ya wale wanaotaka kukutumia na wanao ku support kinafiki. Kama huna marafiki wazuri tafuta uhusiano wa kuomba kama mtanzania mwenzako omba urafiki kama Watanzania walivyokuwa wanafanya miaka ya zamani. Marafiki wabaya watakupeleka jela na kukuingiza kwenye ushabiki wa kimaisha na kukutumia.

4. Acha kulalamika: Kama unataka kuendelea uache utamaduni wa kulalamika badala yake jiulize je ni kitu gani naweza kufanya kufanikiwa bila kuiba. Tabia nzuri inaweza kukupeleka mbali kuliko unavyofikiri pesa pekee sio sababu ya kushidwa kuanza bali mara nyingi ni tabia. Ukiwa na tabia nzuri na kujihusisha na watu wazuri pesa haitakuwa kigezo.

5. Nenda ugaibuni kama umeshidwa yote: Kama yote umeshidwa na mazingira uliyo nayo si mazuri labda kabla ya kujihusisha na biashara haramu jitoe kwenye mazingira uliyopo. Kama bado ni kijana na mambo hayaendi yote hapo juu tafuta njia za kwenda nje lakini hayo mambo hapo juu inabidi uyafuate hata kama uko ugaibuni.

6. Uvumilivu: Hii nitakupa mfano wa ukweli kabisa. Watanzania wengi tulikuwa USA miaka ya 1996-2000 kutafuta maisha kwenda shule n.k. Watanzania wote tuliishi pamoja na mimi nilikuwa mojawapo pale Houston, TX tulifanya kazi pamoja umri ulikwa kama sawa tu kwa ufupi tulianza wote kwenye zero. Baaada ya miaka michache Watanzania wengine walihusisha na biashara, wengine shule, wengine mission town deals. Waliopiga deal walichukua pesa na kukimbia Tanzania na hawa walienda na magari, pesa na walipata wanawake, wanaume wanaowataka nyumbani. Wengi wao walienda bila kumaliza shule au kujifunza biashara.

Waliobaki makundi mawili wanaofanya kazi na kwenda shule na wanaofanya kazi lakini hawaendi shule. Wale walioenda Tanzania wengi wao wameishiwa na hawawezi kuja kwani ni wezi. Wengine walifungwa kabla hata ya kwenda Tanzania na walirudishwa bila kitu. Waliobaki ambao hawakwenda shule ndiyo sasa wanaanzan kwenda shule wakiwa na miaka 35 au zaidi. Walioenda shule hata kama kwa shida wanafanya vizuri sana na community imekuwa na watu wenye mafanikio kiuchumi kuliko community nyingi za Kitanzania duniani. Kuna Watanzania ambao ni VP wa kampuni kuna Watanzania wengi sasa wanatengeneza $50,000 mpaka $120,000 kwa mwaka kwenye mishahara. Hivyo maisha si kuiba tu unaweza kufanikiwa bila kuiba.

Alex Masawe ni tajiri mkubwa sana wa Kitanzania laikini kwasababu kapata utajiri wake kwa kuiba na hata kuua sasa kwenye miaka karibu sabini ndiyo anaenda jela badala ya kutumia pesa alizopata anaenda jela. Serikali inaweza kutaifisha mali zake hivyo uwizi wote huo aliofanya miaka yote ameishia wapi!!. Usisikilize watu wanaokuambia huwezi kufanya kwani si ukweli